NEWS

Wednesday, 4 September 2024

Ukraine katika mchakato wa mabadiliko,mawaziri wajiuzulu





 
Maafisa sita wa Ukraine, wakiwemo wajumbe wa baraza la mawaziri, wamejiuzulu nyadhifa zao kabla ya mabadiliko makubwa ya serikali yanayotarajiwa.

Kujiuzulu huku kunaacha baadhi ya nafasi za kazi serikalini zikiwa wazi, akiwemo waziri wa viwanda wa kimkakati anayehusika na utengenezaji wa silaha.

Mabadiliko hayo yanakuja huku kiongozi wa bunge wa chama tawala cha Servant of the People akisema nusu ya baraza la mawaziri litabadilishwa katika mabadiliko makubwa ya serikali wiki hii.

Mabadiliko hayo yanakuja wakati Ukraine inaendelea kukabiliana na mashambulizi ya kila siku ya Urusi katika miji yake, na inajitahidi kuzuia mafanikio ya Moscow katika eneo la mashariki.

Waliowasilisha kujiuzulu kwao siku ya Jumanne ni pamoja na Waziri wa Viwanda vya Kimkakati, Alexander Kamyshin, Waziri wa Sheria, Denys Maliuska, Waziri wa Ulinzi wa Mazingira, Ruslan Strilets, Naibu Waziri Mkuu, Olha Stefanishyna na Iryna Vereshchuk.

Mmoja wa wasaidizi wakuu wa Rais, Rostyslav Shurma pia alifukuzwa kazi kwa amri ya Rais.
             Chanzo: BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages