NEWS

Tuesday, 29 October 2024

Kura za maoni CCM: Mgombea alia kuhujumiwa kura Tarime Vijijini, akusudia kushitaki kwa Dkt Nchimbi



Matiko Chacha Nyaiho
-------------------------------


Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Kura za maoni ndani ya CCM katika kijiji cha Nyakunguru kilichopo jimbo la Tarime Vijijini, zimeingia dosari baada ya mgombea kudai kuhujumiwa ushindi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Nilishinda kwa kura 744 lakini cha ajabu aliyepata kura 470 ameteuliwa kugombea uenyekiti wa kijiji baada ya kuongezewa kura haramu zikafika 790,” amesema Matiko Chacha Nyaiho katika mazungumzo na Mara Online News kwa njia ya simu leo.

Kutokana na hali hiyo, Nyaiho sasa anachukua hatua ya kuwasilisha malalamiko hayo kwa uongozi wa juu wa chama chake. “Ninaandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuomba uchaguzi urudiwe,” amesema.

Taarifa zilizoifikia ofisi ya CCM Wilaya ya Tarime zinaonesha kuwa Kisiri Mwita Mayeye aliongoza kwa kura 790 dhidi ya Nyaiho (kura 744).

Uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa (vijiji, vitongoji na mitaa) unatarajiwa kufanyika nchini kote Novemba 27, 2024 ambapo vyama mbalimbali vya siasa vitasimamisha wagombea.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages