NEWS

Monday, 28 October 2024

Man United yamtimua Kocha Ten Hag

Kocha Ten Hag aliyefutwa kazi na klabu ya Manchester United
--------------------------

Manchester United imemfuta kazi kocha Erik ten Hag baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka miwili na nusu.

Mholanzi huyo aliarifiwa kuhusu uamuzi huo na bodi ya klabu hiyo Jumatatu asubuhi.

Manchester United imeanza vibaya msimu huu huku mechi ya mwisho ya Ten Hag ikiwa ya Jumapili ambapo Man Utd ilishindwa mabao 2-1 na West Ham.

United pia wako katika nafasi ya 21 kati ya timu 36 kwenye jedwali la Ligi ya Europa, wakiwa wametoka sare katika mechi zao tatu za ufunguzi.

Ruud van Nistelrooy, ambaye alijiunga na klabu hiyo kama msaidizi wa Ten Hag msimu uliopita wa joto, ametajwa kuwa kocha wa muda hadi kocha mkuu wa kudumu atakapoajiriwa.

Klabu hiyo ilikuwa imeongeza mkataba wa Ten Hag kwa mwaka mmoja kufuatia ushindi wa fainali ya Kombe la FA mwezi Mei dhidi ya Manchester City lakini zaidi ya miezi mitatu baadaye amefutwa kazi baada ya kusimamia mwanzo mbaya zaidi wa United wa pili kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

United sasa wanatafuta kocha wao wa sita wa kudumu tangu Sir Alex Ferguson astaafu mwaka 2013.

Kocha wa zamani wa Ajax Ten Hag, 54, alichukua mikoba msimu wa joto mwaka 2022 na kuiongoza klabu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Primia katika msimu wake wa kwanza.

Pia aliiongoza United kutwaa taji lao la kwanza katika misimu sita kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United kwenye fainali ya Kombe la Carabao 2023 na kumaliza washindi wa pili katika fainali ya Kombe la FA, wakifungwa 2-1 na Manchester City.

Msimu wake wa pili kama msimamizi wa klabu hiyo ulianza vibaya, huku United wakimaliza mkiani katika kundi lao la Ligi ya Mabingwa msimu wa vuli lakini wakatwaa kombe, na kuwalaza Manchester City katika fainali ya Kombe la FA.

Kampuni ya Sir Jim Ratcliffe ya Ineos ilinunua asilimia 27.7 ya hisa za klabu hiyo mnamo mwezi Desemba 2023 na bilionea huyo wa Uingereza aliiambia BBC Sport mnamo mwezi Februari matatizo ya klabu hiyo yaliongezeka zaidi ya jukumu la kocha.

"Katika miaka 11 iliyopita, Manchester United imekuwa na makocha wengi na hakuna aliyefanikiwa katika nyanja hiyo," alisema Ratcliffe. "Hiyo kwangu inamaana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa kimazingira."

Lakini mwanzo mbaya wa msimu, ambao umeshuhudia United ikishinda mechi moja tu kati ya nane zilizopita katika mashindano yote, imeilazimu bodi kuchukua hatua.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages