NEWS

Tuesday, 15 October 2024

Mgodi wa North Mara kutumia bilioni 9 kutekeleza miradi ya kijamii Tarime Vijijini




NA MWANDISHI WETU, Tarime
------------------------------------------

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara umepanga kutumia shilingi bilioni tisa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).

Fedha hizo zitagharimia utekelezaji wa miradi 101 kupitia mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) wa mgodi huo.

Meneja Mkuu (GM) wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) walipofanya ziara mgodini hapo wiki iliyopita.

“Miradi hii inasaidia kukuza na kudumisha mahusiano yetu na jamii,” GM Lyambiko alisema.

Awamu iliyopita, mgodi wa North Mara ulitumia shilingi zaidi ya bilioni saba kugharimia utekelezaji wa miradi mingi kupitia mpango wake wa CSR.

Miradi inayotekelezwa na mgodi wa North Mara kupitia mpango huo ni ya sekta za elimu, afya, maji na uchumi.

Katika hatua nyingine, GM Lyambiko alisema idadi ya wafanyakazi wazawa waliopata ajira katika mgodi huo imeongezeka kutoka asilimia 31 hadi 51 kwa sasa.

Aidha, alitaja mafanikio mengine kuwa ni kiasi kikubwa cha fedha kinachotumika kulipa wazabuni na wakandarasi wazawa wanaoupatia mgodi huo huduma mbalimbali, jambo ambalo limeonesha mafanikio katika utekelezaji wa sera ya “local content’.

Waandishi hao pia walipata fursa ya kutembelea baadhi ya miradi ya huduma za kijamii iliyotekelezwa na mgodi huo katika vijiji vinavyouzunguka.

Walitembelea Shule ye Msingi mpya Kenyangi iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.287 na mradi wa kilimo biashara unaoendeshwa na vijana katika kijiji cha Matongo.
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages