NEWS

Wednesday, 16 October 2024

Nyambari ahamasisha Watanzania kujiandikisha kupiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa








Mfanyabiashara,Mwandishi na Mchapishaji maarufu wa vitabu nchini, Nyambari
Nyangwine, akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kujiandikisha kwenye daftari la makazi la wapiga kura kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi ujao Novemba 27.

                                 ----------------

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Mfanyabiashara ,Mwandishi na Mchapishaji wa vitabu maarufu nchini Tanzania, Nyambari Nyangwine, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi ujao Novemba 27.

Nyangwine alitoa wito huo jana baada ya kujiandikisha katika mtaa wake wa Mikocheni jijini Dar es Salaam.




“Naamini ni wajibu wangu na haki yangu kuchagua kiongozi ambaye atatufaa,” Nyangwine ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Tarime kupitia chama tawala- CCM, huku akiweka mkazo kwa Watanzania wa makundi yote katika jamii wajitokeze na kushiriki katika uchaguzi huo na kuitumia fursa hiyo kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Alisema ni muhimu kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu maendeleo katika taifa yanaanzia kwenye ngazi hizo ambako wanaishi mamilioni ya Watanzania.

Zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye uchaguzi huo lilianza rasmi nchini kote Oktoba 11, 2024 na litakamilika Oktoba 20.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages