![]() |
Naibu Rais wa Kenya (aliyesimama) , Rigathi Gachagua akiwa katika moja ya vikao vilivyojadili hoja ya kumtimua madarakani |
-------------------------
Maseneta wa Kenya walipiga kura kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoka ofisini, licha ya kutokuwepo kwake katika kesi ya kumtimua kutokana na kuugua, kulingana na wakili wake. Gachagua alitarajiwa kutoa ushahidi katika Seneti lakini alikuwa amekanusha mashtaka 11 awali.
Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, alitimuliwa kutoka ofisini Alhamisi katika mchakato wa kisiasa usio wa kawaida ambao umeibua hisia mseto kote nchini na hata kimataifa.
Katika hatua ya kihistoria, Seneti ilipiga kura kumtimua Gachagua kwa mashtaka matano kati ya kumi na moja, baada ya pendekezo kama hilo kupitishwa kwa wingi na bunge la chini la Bunge la Kitaifa wiki iliyopita.
Kura hiyo ilifanyika katika siku yenye mvutano mkubwa ambapo Gachagua, mwenye umri wa miaka 59 na anayejulikana kama "Riggy G", alishindwa kutoa ushahidi wa kujitetea baada ya kupelekwa hospitalini kutokana na maumivu makali ya kifua.
Yeye ni naibu rais wa kwanza kutimuliwa kwa njia hii tangu mfumo wa wa kupiga kura ya kumwondoa kiongozi madarakani uanzishwe katika katiba iliyorekebishwa ya Kenya ya mwaka 2010.
Kuanguka kwake ni matokeo ya mzozo mkali na Rais William Ruto, ambaye alisaidia kushinda uchaguzi wa 2022 kwa kuhamasisha msaada kutoka eneo lenye wingi wa kura la Mlima Kenya.
"Seneti imeamua kumwondoa ofisini, kwa kumtimua, Mheshimiwa Rigathi Gachagua, naibu rais wa Jamhuri ya Kenya," alisema Spika wa Seneti Amason Kingi baada ya kura hiyo.
"Kwa hivyo, Mheshimiwa Rigathi Gachagua hawezi tena kushikilia ofisi."
Gachagua alipatikana na hatia kwa mashtaka ya "ukiukaji mkubwa" wa katiba, ikiwemo kufanya siasa za ukabila, lakini alisitishwa kwa mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na ufisadi na kuficha fedha.
Gachagua alikuwa amekanusha tuhuma zote dhidi yake akizielezea kuwa "za kipumbavu" na "za kushtua".
Aidha kwa upande mwingine, Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ajaye kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua Alhamisi usiku.
Jina la Kindiki limewasilishwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.
Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa leo Ijumaa.
Katiba inasema pindi rais anapowasilisha uteuzi kwenye Bunge, wabunge watapiga kura ya kulikataa au kuliidhinisha jina hilo. Pia hakuna sharti la kura ya thuluthi mbili.
“Prof. Kindiki, ambaye kwa sasa anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini kutoka kwa Bunge la Kitaifa kabla ya kushika nafasi ya Naibu Rais. Bunge lazima lipigie kura uteuzi ndani ya siku 60 baada ya kupokea jina hilo.
Baada ya kuidhinishwa, mteule atateuliwa rasmi na Rais kuwa naibu wake. Ingawa Katiba haijaweka bayana muda wa uteuzi huu, unatarajiwa kutokea mara baada ya kuidhinishwa na Bunge.Chanzo:BBC
Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, alitimuliwa kutoka ofisini Alhamisi katika mchakato wa kisiasa usio wa kawaida ambao umeibua hisia mseto kote nchini na hata kimataifa.
Katika hatua ya kihistoria, Seneti ilipiga kura kumtimua Gachagua kwa mashtaka matano kati ya kumi na moja, baada ya pendekezo kama hilo kupitishwa kwa wingi na bunge la chini la Bunge la Kitaifa wiki iliyopita.
Kura hiyo ilifanyika katika siku yenye mvutano mkubwa ambapo Gachagua, mwenye umri wa miaka 59 na anayejulikana kama "Riggy G", alishindwa kutoa ushahidi wa kujitetea baada ya kupelekwa hospitalini kutokana na maumivu makali ya kifua.
Yeye ni naibu rais wa kwanza kutimuliwa kwa njia hii tangu mfumo wa wa kupiga kura ya kumwondoa kiongozi madarakani uanzishwe katika katiba iliyorekebishwa ya Kenya ya mwaka 2010.
Kuanguka kwake ni matokeo ya mzozo mkali na Rais William Ruto, ambaye alisaidia kushinda uchaguzi wa 2022 kwa kuhamasisha msaada kutoka eneo lenye wingi wa kura la Mlima Kenya.
"Seneti imeamua kumwondoa ofisini, kwa kumtimua, Mheshimiwa Rigathi Gachagua, naibu rais wa Jamhuri ya Kenya," alisema Spika wa Seneti Amason Kingi baada ya kura hiyo.
"Kwa hivyo, Mheshimiwa Rigathi Gachagua hawezi tena kushikilia ofisi."
Gachagua alipatikana na hatia kwa mashtaka ya "ukiukaji mkubwa" wa katiba, ikiwemo kufanya siasa za ukabila, lakini alisitishwa kwa mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na ufisadi na kuficha fedha.
Gachagua alikuwa amekanusha tuhuma zote dhidi yake akizielezea kuwa "za kipumbavu" na "za kushtua".
Aidha kwa upande mwingine, Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ajaye kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua Alhamisi usiku.
Jina la Kindiki limewasilishwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.
Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa leo Ijumaa.
![]() |
Profesa Kithure Kindiki aliyeteuliwa kuwa Naibu Rais mpya wa Kenya |
---------------------
Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais kuhusu uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kujaza nafasi katika afisi ya Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya,” Wetang’ula alitangaza.Katiba inasema pindi rais anapowasilisha uteuzi kwenye Bunge, wabunge watapiga kura ya kulikataa au kuliidhinisha jina hilo. Pia hakuna sharti la kura ya thuluthi mbili.
“Prof. Kindiki, ambaye kwa sasa anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini kutoka kwa Bunge la Kitaifa kabla ya kushika nafasi ya Naibu Rais. Bunge lazima lipigie kura uteuzi ndani ya siku 60 baada ya kupokea jina hilo.
Baada ya kuidhinishwa, mteule atateuliwa rasmi na Rais kuwa naibu wake. Ingawa Katiba haijaweka bayana muda wa uteuzi huu, unatarajiwa kutokea mara baada ya kuidhinishwa na Bunge.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>HABARI PICHA:Mahafali ya 12 ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Nyamisangura katika picha
>>MAKALA:Wananchi Nyatwali: Tunaishukuru Serikali kututua mzigo wa adha za tembo
>>HABARI PICHA:Mahafali ya 8 Sekondari ya JK Nyerere yalivyofana katika picha, MNEC Joyce Mang'o awa mgeni rasmi, CEO Mara Online akabidhi vitabu
>>MAKALA MAALUMU:Tunamuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuwafikishia wananchi huduma ya maji, hakuna atakayeachwa
No comments:
Post a Comment