NEWS

Saturday, 19 October 2024

Mahafali ya 8 Sekondari ya JK Nyerere yalivyofana katika picha, MNEC Joyce Mang'o awa mgeni rasmi



Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa, Joyce Ryoba Mang'o akiwasilisha hotuba yake kama mgeni rasmi katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari JK Nyerere iliyopo Tarime Vijijini jana Oktoba 18, 2024. Wengine ni Mwenyekiti wa UWT CCM Wilaya ya Tarime, Neema Charles (mwenye miwani anayepiga makofi), Diwani wa Kata ya Nyamwaga, Mwita Magige (kulia) na Mkuu wa Shule hiyo, Melesian Julius Gerald (kushoto).


Mgeni rasmi MNEC Joyce Mang'o (kushoto mbele) akipokewa na Diwani wa Kata ya Nyamwaga, Mwita Magige kushiriki Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari JK Nyerere jana Oktoba 18, 2024.


Mgeni rasmi MNEC Joyce Mang'o akiungana na wenyeji wake wakiwemo wanafunzi, wazazi na walimu kucheza muziki wakati wa Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari JK Nyerere jana Oktoba 18, 2024.


Sehemu ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari JK Nyerere wakiimba na kucheza kwa madaha wakati wa mahafali yao shuleni hapo jana Oktoba 18, 2024.


Mgeni rasmi MNEC Joyce Mang'o akihamasisha na kuongoza changisho la fedha katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari JK Nyerere ili kununua ng'ombe wa nyama kwa ajili ya wanafunzi hao shuleni hapo jana Oktoba 18, 2024.

Pamoja na mambo mengine, MNEC Joyce Mang'o aliahidi kusaidia kutatua changamoto ya maji katika shule hiyo kwa kutoa shilingi zaidi ya milioni 20 kugharimia uchimbaji wa kisima.


CEO wa Mara Online, Jacob Mugini (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Shule ya Sekondari JK Nyerere wakati akimkabidhi msaada wa vitabu vya kidato cha tano na sita uliotolewa na Taasisi ya Nyambari Nyangwine (NNF) shuleni hapo jana Oktoba 18, 2024. Aliyeshikilia sehemu ya vitabu hivyo ni MNEC Joyce Mang’o.


Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari JK Nyerere wakifurahia maneno ya CEO wa Mara Online, Jacob Mugini wakati wa kukabidhi msaada wa vitabu uliotolewa na Taasisi ya Nyambari Nyangwine (NNF) shuleni hapo jana Oktoba 18, 2024.


Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Jk Nyerere, Melesian Julius Gerald, CEO wa Mara Online, Jacob Mugini, Diwani wa Kata ya Nyamwaga, Mwita Magige, MNEC Joyce Mang'o na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wakionesha sehemu ya msaada wa vitabu uliotolewa na Taasisi ya Nyambari Nyangwine (NNF) shuleni hapo jana Oktoba 18, 2024. (Picha zote na Mara Online News)
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages