NEWS

Tuesday, 22 October 2024

Watu wanane waripotiwa kufariki dunia katika ajali ya mabasi Mwanza




Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Watu wanane wameripotiwa kufariki dunia na wengine 39 kujeruhiwa baada ya mabasi ya abiria ya Nyehunge na Asante Rabi kugongana leo alfajiri katika eneo la Ukirigulu, Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha tukio hilo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni basi la Asante Rabi lenye namba za usajili T 458 DYD lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Arusha kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari, kitendo kilichosababisha kugongana na basi la Nyehunge lililokuwa linatokea Morogoro kwenda Mwanza.

Kamanda Mutafungwa ametoa wito wa kuwataka madereva kuwa waangalifu zaidi barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima zinazotokana na mwendokasi na uzembe.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages