NEWS

Saturday, 26 October 2024

Waziri Mkuu Majaliwa akabidhi magari mapya kwa TAKUKURU




Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ambayo yatasambazwa mikoani kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo ya umma.

Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195, kati ya hayo, 88 yameshanunuliwa.

“Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu” amesema Crispin.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya TAKUKURU katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 26, 2024.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages