
Tundu Lissu akihutubia mkutano wa kampeni za CHADEMA mjini Tarime jana.
---------------------------------------
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa (Bara), Tundu Lissu jana alihutubia mikutano ya kampeni akiwaombea kura wagombea wanaopeperusha bendera ya chama hicho.
Mikutano hiyo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika eneo la Nyamongo [Tarime Vijijini] na Tarime Mjini.
Lissu aliwaomba wananchi wa maeneo hayo kuwachagua wagombea wanaotokana na chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao umepangwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Tundu Lissu (katikati) akipungia mkono wananchi kwenye mkutano wa Nyamongo.
------------------------------------------
"Ukizungumza na mwenzako yeyote mwambie jukumu letu la kwanza ni kuhakikisha wagombea wetu wote wanashinda,” alisema Lissu katika sehemu ya hotuba yake akiwa Nyamongo.
Baadaye jioni, Lissu alihutubia mkutano mkubwa wa CHADEMA katika mji wa Tarime ambapo pia aliwaombea kura wagombea kutoka chama hicho cha upinzani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wenye maono ya maendeleo.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Barrick North Mara, Biashara United Veterani zachuana mechi za kirafiki Nyamongo
>>Barrick yatunukiwa tuzo ya kudhamini mkutano wa kimataifa wa madini
>>Biteko awatajia wananchi 'viongozi wa maendeleo' akizindua kampeni za CCM Mara
>>Mfanyabiashara wa Tanzania Nyambari Nyangwine sasa kuwekeza Uganda
No comments:
Post a Comment