NEWS

Saturday, 23 November 2024

Watu wanne wafa katika ajali ya lori lililoparamia vibanda vya biashara Bunda




Na Mwandishi Wetu, Bunda

Watu wanne wameripotiwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya lori aina ya Fuso lililokuwa limebeba mawe kufeli breki na kuparamia jengo lenye vibanda vya biashara mjini Bunda, Mara.

Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana Novemba 22, 2024 saa 5:00 asubuhi katika makutano ya barabara za Nyamuswa-Ukerewe na Musoma-Mwanza.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Dkt Yusufu Wambura alithibitisha Hospitali ya Teule ya Wilaya ya Bunda kupokea miili ya watu wanne na majeruhi sita na kwamba baadaye mmoja aliwahishwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa Dkt Wambura, mmoja wa majeruhi alilazimika kukatwa mguu kutokana na majeraha makubwa, huku mwingine akifanyiwa upasuaji.

Mbali na kusababisha vifo na majeruhi, ajali hiyo pia iliharibu mali mbalimbali za wafanyabiashara.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages