NEWS

Monday, 23 December 2024

Ajali ya basi yakatisha maisha ya watu 11 Biharamulo



Waziri Innocent Bashungwa akimjulia hali majeruhi katika Hospitali Teule ya Biharamulo juzi.
----------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Biharamulo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewajulia hali majeruhi wa ajali ya basi iliyosababisha vifo vya watu 11 wilayani Biharamulo, Kagera.

Bashungwa alikwenda kuwajulia hali majeruhi hao katika Hospitali Teule ya Biharamulo juzi, baada ya kutembelea eneo la Bukombe katani Nyarubango ilipotokea ajali hiyo ya basi lenye namba za usajili T 857 DHW.

Basi hilo ambalo lilikuwa linatoka Kigoma kwenda Bukoba lilisimama kushusha abiria, kisha likashindwa kuondoka na kuanza kurudi nyuma ambapo liliacha njia na kupinduka.

“Nitumie nafasi hii kuombea raho za marehemu ambao tumewapoteza katika ajali ambayo imetokea hapa Biharamulo, tumepoteza ndugu zetu 11, wametangulia mbele za haki” alisema Waziri Bashungwa

Alisema wizara yake imeanza kufanyia kazi maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfumo wa leseni za udereva ili kuwapunguzia alama hadi kuwafungia madereva wanaofanya makosa ya kuhatarisha usalama barabarani.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Biharamulo, Dkt Gresmus Sebuyoya, watu waliokufa katika ajali hiyo ni wanawake watano, wanaume wanne na watoto wawili.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages