
Na Mwandishi Maalumu/ Mara Online News
Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mara (WAACU Ltd) kimeibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwa uzalishaji wa kahawa bora kwa mwaka 2024/202, kikivibwaga vyama vyenzake 11.
Nafasi ya pili imechukuliwa na BURKA COFFFEE ESTATE cha mkoani Arusha, huku FINAGRO PLANTATION pia cha mkoani humo ikishika nafasi ya tatu.
Mashindano hayo yalifanyika Desemba 16 hadi 20, mwaka huu katika viwanja vya Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) makao makuu Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Siri ya mafanikio ya ushindi huo wa WAMACU ni uwezesho mkubwa ambao WAMACU inaupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kwa mujibu wa Meneka Mkuu (GM) wa ushirika huo, Samwel Marwa Gisiboye.
Ushirika wa WAMACU umekuwa ukitwaa makombe kitaifa kwa kuwa mzalishaji wa kahawa bora yenye muonjo na ladha nzuri kwa miaka kadhaa mfulilizo sasa.

Meneja Shughuli na Biasahra wa WAMACU Ltd, Olais Piniel akiwa na Tuzo ya ushindi wa uzalishaji wa kahawa bora.
----------------------------------
Wakulima wa Mara wanazalisha kahawa aina ya Arabica ambayo inalimwa kwa wingi katika wilaya ya Tarime, kaskazini-mashariki mwa mkoa wa Mara.
Kahawa hiyo pia inaripotiwa kuendelea kutamba katika soko la dunia, na hivyo kuchangia kuliingizia taifa fedha za kigeni.
WAMACU wamendelea kuboresha huduma kwa wakulima wa kahawa na mazao megnine kama vile mahindi na tumbaku mkoani Mara.

Chama hicho kinajishughulisha na ukusanyaji wa kahawa kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kuiongezea thamani na kuitafutia masoko nje ya nchi.
Meneja Mkuu wa WAMACU Ltd, Gisiboye, aliiambia Mara Online News kwamba ushindi walioupata ni fahari kubwa kwa wakulima wa kahawa mkoani Mara.
WAMACU pia wana leseni ya kuuza kahawa moja kwa moja katika soko la dunia, baada ya kuikusanya kutoka kwa wakulima kupitia Vyama vya Msingi vya Masoko na Ushirika (AMCOS)na kuiuza katika masoko mbalimbali nje ya Tanzania kama vile Uingereza na Marekani.

Pia kahawa ya Arabica inayolimwa Tarime inauzika vizuri katika nchi za Uholanzi, Ugiriki, Uhispania, Ujerumani, Costa Rica na Colombia, kwa mujibu wa GM Gisiboye.
Oktoba mwaka jana, ushirika wa WAMACU uliibuka mshindi wa Tuzo ya Chama Bora cha Ushirika katika Usambazaji wa Mbobelea Kanda ya Ziwa.
Tuzo hiyo ilitolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
WAMACU Ltd ni miongoni mwa Vyama Vikuu vya Ushirika vilivyopewa dhamana ya kusimamia usambazaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima kwa kushirikiana na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), TFC na OCP.
Pia, kwa sasa ushirika wa WAMACU una leseni ya uwakala wa kusambaza pembejeo ikiwemo mbolea kutoka TFRA.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Ajali ya basi yakatisha maisha ya watu 11 Biharamulo
>>Aliyewahi kuwa RC, Naibu Waziri ampongeza Rais Samia kwa kazi nzuri, amtabiria ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao
>>Mara Press haitafanya kazi na online TV, blogs ambazo hazijasajiliwa TCRA – Mugini
>>TAMISEMI yatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2025
No comments:
Post a Comment