NEWS

Sunday, 1 December 2024

Man Utd yamruhusu Rashford kuondoka

Marcus Rashford

MANCHESTER United imemruhusu mshambuliaji wa Uingereza, Marcus Rashford,27, kuondoka kwa uhamisho.

Wakati huo huo, Manchester United hawana uwezekano wa kumpa ChristianEriksen, 32, mkataba mpya, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Denmark ukikamilika mwishoni mwa msimu.

Kwa upande wake winga wa Liverpool, Federico Chiesa, 27, anafikiriwa na Napoli ili kuchukua nafasi ya Khvicha Kvaratskhelia, ikiwa mshambuliaji huyo wa Georgia hatatia saini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Serie A.
Federico Chiesa
Juventus wao wanafikiria kumnunua Liam Delap wa Ipswich na wametuma maskauti kumtazama mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia anazivutia Chelsea na Manchester United.

Klabu hiyo ya Italia pia inatazamia kumnunua mshambuliaji wa Manchester United kutoka Uholanzi, Joshua Zirkzee, 23, kwa mkopo.

Naye kiungo wa kati wa Uhispania, Dani Ceballos, 28, anaweza kuwa njiani kuondoka Real Madrid, huku Real Betis wakiwa na nia ya kumrejesha mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal katika klabu hiyo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages