NEWS

Sunday, 1 December 2024

Ruto aahidi kuimarisha uchumi Afrika Mashariki

William Ruto
Na Mwandishi Wetu, Arusha
----------------------------------------

 
Rais William Ruto wa Kenya Jumamosi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuchukua nafasi ya Rais Salvar Kiir wa Sudani Kusini aliyemaliza muda wake huku akiahidi kuimarisha uchumi wa eneo hili linaloshuhudia kasi ya ongezeko la wawekezaji kutoka nje.

Nafasi ya Mwenyekiti wa EAC inakwenda kwa mzunguko baina ya nchi nane wanachama wa jumuiya hiyo ambayo inapata mafanikio ya kukua kwa biashara ya nchi wanachama.
Rais Ruto alichaguliwa wakati wa Mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki.

Mkutano huo uliteua Jamhuri ya Shirikisho la Somalia kuwa Ripota wa EAC kwa mwaka ujao.Uchaguzi huo ulifanywa na marais wa nchi za EAC za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda, Sudan Kusini na Somalia.
 
Baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Ruto aliahidi kwamba kazi kubwa inayomkabili itakuwa ni kuimarisha uchumi wa Afrika Mashariki kwa kukusanya juhudi za pamoja za nchi wanachama.

Afrika Mashariki kwa sasa ndilo eneo linaibuka kiuchumi kwa kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali za na kushindana na maeneo mengine ya jumuiya za maendeleo Afrika.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages