NEWS

Sunday, 29 December 2024

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter afariki akitimiza miaka 100



Plains Georgia -


Rais wa zamani wa Marekani aliyeishi kwa muda mrefu kuliko marais wote wa nchi hiyo, Jimmy Carter, amefariki dunia nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 100, kwa mujibu wa familia yake na kituo chake cha Carter  Centre.


Taarifa iliyotolewa kwenye mitandao na kituo cha Carter Centre ilisema: "Muasisi wetu na Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, amefariki mchana huu huko Plains Georgia."


"Baba alikuwa shujaa, siyo tu kwangu, bali kwa kila mmoja anayeamini katika amani, haki za binadamu na upendo usiyo na choyo," alisema Chip Carter, mtoto wa kiume wa rais huyo wa zamani  katika taarifa ya mtandao wa Carter Centre.


"Kaka zangu, dada yangu na mimi mwenyewe tuliishi na dunia tukiwa na imani hizi. Dunia ndiyo familia yetu kwa jinsi alivyotuleta pamoja, na tunashukuru kwa kuheshimu kumbukumbu yake kwa kuzingatia imani hizi."


Carter, ambaye alikuwa ni mwanachama wa Democrat, alikuwa Rais wa Marekani wa 39 kutoka mwaka 1976 mpaka 1981.


Anajulikana sana kwa kazi yake ya kujali ubinadamu baada ya kuondoka Ikulu ya Marekani, ikiwemo kujishughulisha na suala la Makazi kwa Binadamu na mikataba ya amani.


Ramnirambi kwa kifo cha Rais Carter zilianza kumiminika Jumapili zikiwemo kutoka kwa Rais Mteule, wa Marekani, Donald Trump, ambaye alisema "Baadhi yetu ambao tulibahatika kuwa Rais, klabu hii ni ya kipekee, tunaelewa kazi kubwa ya kutumikia Taifa Letu Kubwa katika Historia yake." 


"Changamoto alizokumbana nazo Rais Carter zilikuja kwenye wakati muhimu wa taifa letu na alijitahidi kuboresha maisha ya Wamarekani. Kwa jambo hilo tunawiwa deni kubwa la shukrani kwa Rais Carter."

Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages