NEWS

Friday, 3 January 2025

Chandi ataka utoroshaji wa tumbaku udhibitiwe



 
NA MWANDISHI WETU
-----------------------------------

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (pichani) ametaka utoroshaji wa tumbaku kwenda nchi jirani udhibitiwe, ili kuokoa mapato ya serikali yanayotokana na biashara ya zao hilo.
 
“Baadhi ya tumbaku inayolimwa mkoani Mara inatoroshwa kwenda nchi jirani na kuikosesha serikali mapato yanayotokana na mauzo ya zao hilo,” alisema Chandi wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara, uliofanyika Jumatatu iliyopita mjini Tarime.
 
Aliendelea: “Mamlaka husika zidhibiti tatizo hili serikali ikusanye mapato. Wafanyabiashara kutoka nje ya nchi walazimike kuja kununua tumbaku kwa njia halali - hata kwa Dola za Kimarekani ili wakulima wanufaike zaidi.”
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages