NEWS

Tuesday, 14 January 2025

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi afariki dunia, Rais Samia amlilia



Ester Alexander Mahawe enzi za uhai

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Godfrey Chongolo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Alexander Mahawe.

Mahawe amefariki dunia leo Januari 14, 2025 katika Kospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

“Rais Dkt Samia anawapa pole familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mahawe. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mahawe mahala pema peponi, Amina,” imesema sehemu ya taarifa ya serikali kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Sharifa Nyanga, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Mahawe aliteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mwaka 2023.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages