NEWS

Friday, 17 January 2025

Safari za anga zarejeshwa viwanja vya Serengeti Kusini na Lobo katika Hifadhi ya Serengeti



Ndege iliyobeba watalii ikielekea kutua ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeidhinisha kurejeshwa kwa safari za anga kwa viwanja vya Serengeti Kusini na Lobo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) anayeshughulikia Mawasiliano, Catherine Mbena, kurejea kwa safari za anga katika hifadhi hiyo maarufu duniani kunafuatia kukamilika kwa ukarabati na matengenezo ya viwanja hivyo.

Mbena alisema katika taarifa hiyo Januari 14, 2025 kwamba viwanja vyote saba katika Hifadhi ya Serengeti vinafanya kazi, na safari zote katika hifadhi hiyo sasa ni salama.

“Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu katika kipindi hiki cha matengenezo na ukarabati, na tunawatakia safari njema wakati wa kupaa na kutua katika hifadhi hii inayoongoza kwa ubora barani Afrika,” alisema.

Hifadhi ya Serengeti ni moja ya maeneo maarufu duniani yenye maajabu ambayo yanalindwa na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages