NEWS

Thursday, 16 January 2025

Mwenyekiti mpya MISA Tanzania awatembelea wadau wa habari Kanda ya Ziwa



Mwenyekiti mpya wa MISA-Tan, Edwin Soko akizungumza na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Imilda Sulum alipomtembelea meneja huyo ofisini kwake jijini Mwanza leo Januari 16, 2025.
-----------------------------------

Mwandishi Wetu, Mwanza

Mwenyekiti mpya wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika upande wa Tanzania (MISA-Tan), Edwin Soko leo Januari 16, 2025 amefanya ziara ya kujitambulisha katika Mamlaka ya Uthibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Uthibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa.

Katika ziara hiyo, Soko amekutana na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandishi Imelda Salum na kujadilili namna ya kufanya kazi kwa pamoja, ikiwemo kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025 ili wafanye kazi kwa weledi zaidi.

Kwa upande wake Mhandishi Imelda ameipongeza MISA-Tan kwa kuona umuhimu wa kuwa karibu na wadau mbalimbali wa habari, na kusisitiza kuendelea kufanya kazi na wanachama wa taasisi hiyo na waandishi wa habari kwa ujumla nchini.

Kwa upande mwingine, Soko amekutana na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina na kujadiliana juu ya umuhimu wa MISA-Tan katika kusimamia weledi ndani ya taaluma ya habari.


Mwenyekiti mpya wa MISA-Tan, Edwin Soko (kushoto) akiwa na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina alipomtembelea meneja huyo ofisini kwake jijini Mwanza leo Januari 16, 2025.
-----------------------------------

Mhina amesema EWURA iko tayari kushirikiana na MISA-Tan katika kufanya kazi kitaaluma ili kusaidia kupatikana kwa habari jengefu.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa Mwenyekiti huyo mpya wa MISA-Tan kujitambulisha kwa wadau mbalimbali na kuongeza uwigo wa kufanya kazi kwa pamoja.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages