
Prince Karim Al-Hussaini "Aga Khan IV"
Na Mwandishi Wetu
Kiongozi wa 49 wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ismailia duniani, Prince Karim Al-Hussaini anayefahamika kama Aga Khan IV, alifariki dunia juzi Jumanne nchini Ureno akiwa na umri wa miaka 88.
Prince Karim Aga Khan alikuwa mzaliwa wa ukoo wa Mtume Muhammad (SAW) na Muasisi na Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan.
Prince Rahim Al-Hussaini Aga Khan V ameteuliwa kuwa kiongozi wa 50 wa mamilioni ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia duniani kurithi nafasi ya baba yake.
Uteuzi huo ulifanyika baada ya kufunguliwa kwa wosia wa Prince Karim, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Maendeleo la Aga Khan.
Wakati wa uhai wake Prince Karim Al-Hussaini alijitolea kuboresha maisha ya watu na jamii mbalimbali bila kujali madhehebu ya dini au asili ya mtu.
No comments:
Post a Comment