
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Jenerali (Mstaafu) George Waitara (kulia) akifuatilia jambo na wajumbe wa bodi hiyo walipokutana katika kikao chao cha 209.
----------------------------------
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jenerali (Mstaafu) George Waitara imehitimisha kikao chake cha 209 jana Machi 14, 2025 kilicholenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya shirika.
Kikao hicho kilitanguliwa na vikao vya Kamati ya Ukaguzi na Utawala Bora inayoongozwa na CPA Hadija Mohamed Ramadhani, Kamati ya Himasheria na Usimamizi wa Hifadhi inayoongozwa na Dkt Robert Fyumagwa na Kamati ya Utalii na Huduma za Shirika inayoongozwa na Dkt Rhimo Nyansaho.
Aidha, Bodi ilifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara za Banagi - Lobo - lango la Kleins yenye urefu wa kilomita 72 na Golini - Naabi - Seronera (kilomita 68), na ujenzi wa uwanja wa Golf “Serengeti National Park Golf Course” inayotekelezwa na kampuni tanzu ya TANAPA “TANAPA Investment Limited (TIL)”, pamoja na ujenzi wa lango la Kleins unaotekelezwa na kampuni ya Stance Technic and Civil Engineers Limited.
No comments:
Post a Comment