
Mchungaji wa Kanaisa la SDA Mtaa wa Nyabitocho, Kumba Kihiri (kulia) akipokea kutoka kwa Nyambari Nyangwine mchango wa shilingi milioni tano taslimu kwa ajili ya ujenzi wa kibweta cha makambi cha kanisa hilo.
----------------------------------------
Mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini Tanzania, Nyambari Nyangwine, ameendelea kuwa mfano bora, kwa kuonesha upendo wa dhati na moyo wa kujitolea kuchangia maendeleo ya jamii, zikiwemo shughuli za kiroho na kiimani.
Wiki iliyopita, Nyambari ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara mwaka 2010 hadi 2015 kupitia chama tawala - CCM, aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la SDA Nyabitocho wilayani Tarime na kufanikisha kiasi cha shilingi milioni 18.6 kupatikana.
Siku iliyofuata, Nyambari aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Mennonite Mangucha, ambapo jumla ya shilingi milioni 27 zilipatikana. Mchango huo ni uthibitisho wa mapenzi ya kweli aliyonayoa Nyambari kwa maendeleo ya wana-Tarime.
Zaidi ya hayo, Nyambari aliichangia kwaya ya Kanisa la EAGT Sirari shilingi milioni mbili, na pia alilichangia Kanisa la SDA Kyoruba shilingi milioni mbili.
Jumla ya kiasi cha fedha kilichopatikana katika matukio hayo ya Nyambari ni shilingi takriban milioni 50.
Mchango huo wa Nyambari una maana kubwa kwani fedha hizo zitasaidia kuchochea maendeleo ya kiroho kwa waumini na kuwezesha makanisa hayo kutimiza malengo yao ya kiimani na kijamii.
Hatua hizi zinaonesha kuwa Nyambari anajali maendeleo ya kiroho na ustawi wa jamii ya Tarime, na pia anaelewa umuhimu wa kushiriki shughuli zinazosaidia kujenga upendo, umoja na amani katika jamii.
Kwa ujasiri na upendo mkubwa, Nyambari aliendelea kuonesha moyo wa kujitolea pale alipotoa ahadi ya kutoa shilingi milioni 12 kwa makanisa mengine manne ya Romani Katoliki, Anglikana, KKKT na SDA yaliyopo kata ya Nyanungu.
Mchango huo utasaidia sana katika kuimarisha makanisa hayo na kuongeza nguvu zaidi katika kukuza maendeleo ya kiroho na kijamii katika maeneo hayo.

Askofu Amos Mohagaji wa Kanisa la Mennonite Dayosisi ya Shirati akimshukuru Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) kwa kufanikisha harambee ya kuchangia katika Kanisa la Mennonite Mangucha katani Nyanungu.
-------------------------------------
Makanisa yana mchango mkubwa katika jamii. Si tu kwamba ni mahali pa ibada, bali pia ni sehemu muhimu ya kuwaimarisha watu kiimani na kiroho. Vilevile, makanisa hutoa fursa kwa watu kujumuika pamoja na kujenga uhusiano mzuri wa kijamii.
Mchango wa Nyambari katika shughuli hizi unachangia moja kwa moja katika kuhakikisha kuwa makanisa haya yanakuwa na uwezo wa kutimiza majukumu ya kiroho na kijamii.
Kujitolea huku kwa Nyambari hakutawaza tu kutoa mafanikio katika ujenzi wa makanisa, bali pia kutaleta mabadiliko chanya katika jamii ya Tarime kwa kuimarisha upendo, umoja na amani.
Katika hatua hizo za kuchangia ujenzi wa nyumba za Mungu, Nyambari Nyangwine ambaye amewahi kuwa ameonesha kuwa upendo wa kweli unadhihirishwa kwa matendo na si kwa maneno matupu.
Kwa hivyo, ni dhahiri kuwa Nyambari ni kiongozi aliyejaa upendo na kujitolea. Anathibitisha kuwa maendeleo ya kiroho na kijamii yanahitaji juhudi za pamoja, na kuwa kila mtu ana jukumu la kutoa mchango wake kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Hivyo, Nyambari Nyangwine anastahili pongezi kubwa kwa kazi nzuri anayofanya katika kuunga mkono shughuli za kiroho wilayani Tarime, kwani michango yake hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa jamii nzima.
Basi, itoshe tu kusisitiza kuwa Nyambari Nyangwine ni mtu wa watu, ameonesha upendo wa hali ya juu kwa wananchi wa Tarime, na ni mfano bora wa kuigwa na watu wengine katika jamii. Apewe maua yake.

No comments:
Post a Comment