NEWS

Friday, 14 March 2025

Wasira aanza ziara ya kukagua shughuli za CCM Songwe



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira (wa kwanza kulia waliovaa mashati ya kijani) akipokewa na viongozi mbalimbali alipowasili mkoani Songwe jana.
-----------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Songwe

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira, jana Alhamisi aliwasili mkoani Songwe kuanza ziara ya siku tatu ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na chama hicho tawala.

Hiyo ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo mkoani Songwe, baada ya kuchaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kushika wadhifa huo Januari mwaka huu, akichukua nafasi ya Abdulrahman Omar Kinana aliyejiuzulu Julai mwaka jana.

Wasira ni mmoja wa vijana wa Tanzania ambao mwishoni mwa mwaka 1950 akiwa na umri wa miaka 16 alijiunga na harakati za kumng’oa mkoloni, akiunga mkono jitihada za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na waasisi wengine wa chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika cha TANU.

Alipowasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe, Wasira alilakiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na serikali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo.

Mkoa wa Songwe unasifika kwa shughuli za kilimo, ukiwa katika kundi la mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inayozalisha mazao ya chakula kwa wingi. Mikoa hiyo ni Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Katavi na Ruvuma.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages