NEWS

Saturday, 15 March 2025

Taasisi ya Mwanzo Mpya yafuturisha Waislamu Msikiti wa Masjid Sunni Tarime



Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanzo Mpya, Musa Ryoba (kulia aliyevaa kanzu) akikabidhi boksi zenye tende za futari kwa Sheikh wa Wilaya ya Tarime, Masoud Said Wambura leo.
---------------------------------

Na Godfrey Marwa, Tarime

Taasisi ya Mwanzo Mpya yenye makao makuu mkoani Shinyanga, leo Machi 15, 2025 imetoa tende boksi 43 kwa ajili ya futari kwa waumini wa kiislamu katika msikiti wa Masjid Sunni wa wilayani Tarime, Mara.

"Tumetoa sadaka hii kuonesha ari yetu ya umoja, juhudi zetu tunazoweza kufanya walau kusaidia ndugu zetu waliofunga, tunaalika wadau wengine nje na ndani ya Tarime ili tuweze kuungana kuwafanya wenzetu mwezi wao kuisha salama," amesema Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Musa Ryoba wakati akikabidhi msaada huo.

Ryoba ameongeza: "Tukiwa na wimbo mmoja amani yetu iwe tunu katika kudumisha Tarime ambayo ina nuru ya kesho, amani idumishwe ndani ya wilaya yetu na taifa, iwe ndio wimbo na desturi yetu hata baada ya mfungo huu, tukidumisha upendo tutapokea wageni wengi."


Waumini wakigawiwa tende

Naye Sheikh wa Wilaya ya Tarime, Masoud Said Wambura, akito neno la shukrani kwa taasisi hiyo amesema: "Tunashukuru kwa sadaka hii, nimefarijika, nimefurani sana kwa hili ndugu zetu Mwanzo Mpya Foundation kuona kuwa kuna ndugu hapa Tarime waliofunga wakatuletea futari.

"Mtume anatueleza kuwa sadaka iliyokuwa bora ni ile inayotolewa ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani, mmefanya jambo ambalo ni bora. Mwenyezi Mungu akupeni hidaya na kuwatengenezeeni mambo yenu."


Pia, taasisi hiyo imechangia saruji mifuko 50 kwa ajili ya msikiti mpya unaoendelea kujengwa katika eneo la ofisi za BAKWATA mjini Tarime.

"Mtu mwema ni yule anayekumbuka kwao, tumekuta shughuli inaendelea, ni jambo la kushikana mkono katika msikiti huu, tunaomba heri na baraka uishe salama,” amesema Ryoba.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages