NEWS

Friday, 21 March 2025

Kazi na Utu: Urithi wa JPM na mustakabali wa taifa letu



Paul Chacha Makuri

Katika safari ya maendeleo ya taifa letu, tunakumbuka na kuenzi mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi tu” - kipindi cha mwaka 2015 hadi Machi 2021 - ambacho kiliongozwa na viongozi walioacha alama isiyofutika katika historia yetu.

Urithi wa JPM umeweka misingi thabiti ya maendeleo, kupitia utumbutu wake wa kuanzisha miradi mikubwa kama Bwawa la Mwalimu Nyerere, SGR, Daraja la Kigongo - Busisi, uamuzi mgumu wa kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, pamoja na miradi mingi ya kijamii, ukiwemo ujenzi wa shule, hospitali na miradi mingi ya Barabara, n.k.

Tunaposherekea kumbukizi ya miaka minne tangu kuondoka Kwa JPM hapa duniani, tunajivunia maisha yake na mafanikio ya uthubutu wake, na yanatufundisha umuhimu wa umoja, bidii na kujitolea katika kujenga mustakabali bora kwa vizazi vijavyo. Asante JPM.

Tunapoangazia miaka mnne ya Serikali ya Awamu ya Sita - kutoka tarehe 19 Machi 2021 hadi sasa - tumeona pia mabadiliko makubwa yenye nguvu chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan, akichochea sera ya “Kazi Iendelee.”

Uongozi wake umejikita katika kuendeleza na kuimarisha urithi wa JPM kwa kuendeleza na kukamilisha miradi yote muhimu iliyoasisiwa na Awamu ya Tano, huku akileta ubunifu katika sekta mbalimbali za maisha ya wananchi wetu.

Dkt Samia amejidhatiti kuhamasisha maendeleo endelevu, kuimarisha miundombinu na kuboresha huduma za kijamii, na kwa hilo amefanikisha maendeleo ya hali ya juu katika kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi wake mahiri. Anasitahili pongezi na kuungwa mkono.

Katika muktadha wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ni muhimu kwetu sisi wote kama Watanzania kwa ujumla, kuungana kwa umoja wetu na kujiandaa kwa moyo mkunjufu wa kumchagua tena Dkt Samia.

Wito huu sio tu wa kuthamini mafanikio yaliyopita bali pia ni wa kujitayarisha katika kuchukua hatua ya kuendeleza mabadiliko na ustawi wa taifa letu.

Ni wito wa kuenzi mema yote yaliyofanywa ya kuimarisha mazingira ya kazi na maisha ya wananchi, ambayo yamejengwa kwa bidii na kujitolea kwa viongozi wetu wa awali, na sasa ni jukumu letu kuhakikisha tunawaenzi na kuyaendeleza mafanikio hayo.

Tukiangalia urithi wa JPM, tunajifunza kuwa maendeleo ya kweli yanatokana na dhamira ya kujitolea, uadilifu na umoja wa kitaifa. Dkt Samia amejitolea kuendeleza urithi huo, akitumia mafunzo ya awamu iliyopita kama mwongozo wa kujenga mustakabali wa taifa letu.

Ni wakati wa kuhamasisha hisia za umoja na kuwakaribisha wote kushiriki katika kujenga taifa letu kwa moyo mmoja. Tuchukue jukumu hili kwa umakini na tuchague uongozi ambao unaonesha dhamira thabiti ya “Kazi na Utu” - uongozi ambao unazingatia maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.

Tunawasihi wananchi wote kujiandaa, kuhamasika na kuwa sehemu ya mabadiliko haya ya maendeleo. Tuwe na imani kwamba kwa kumchagua tena Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 tutaweza kuendelea kuenzi na kuendeleza mema yaliyoanzishwa katika kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi wake mahiri.

Hivyo basi, wito wetu ni wa umoja na ustawi wa taifa - tukisimamia maendeleo, tukithamini urithi na kuendelea kujenga mustakabali unaowakilisha matakwa na ndoto za kila mwananchi wetu.

Kwa pamoja, tukiwa wamoja katika dhana ya “Kazi na Utu,” tutaendelea kusonga mbele na kujenga taifa letu kwa njia bora zaidi.

Tuchague uongozi unaoleta matumaini, maendeleo na amani kwa wote.

“Kazi na Utu, Tunasonga Mbele”

Paul Chacha Makuri
17 Machi, 2025.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages