
Madiwani wakimsindikiza Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kibweta cha makambi cha Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Nyabitocho katani Mbogi, Tarime Vijijini hivi karibuni.
-------------------------------------
Mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini Tanzania, Nyambari Nyangwine, ameendelea kuwa gumzo na kivutio kikubwa mithili ya lulu kwa wananchi wengi mkoani Mara, hata kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Wananchi hao, wakiwemo vijana, wanawake na wazee wameonesha shauku na matamanio makubwa ya kuona Nyambari ambaye pia ni kada wa chama tawala - CCM, akijitokeza kuomba ubunge katika majimbo yao.
Wamemtaja Nyambari kama kipenzi cha watu wengi ambaye ameonesha uthubutu na moyo wa kujitolea kuchangia maendeleo ya jamii kupitia misaada ya kijamii na kiuchumi, na ambaye amejenga ushirikiano mzuri na wananchi mbalimbali.
Wananchi wengi wamesisitiza katika mahojiano na Sauti ya Mara kuwa Nyambari ni mtu anayeonesha kujali na kushughulikia maendeleo ya jamii bila ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kikoo, kikabila na kidini.
Wananchi hao kutoka majimbo ya Tarime Vijijini, Tarime Mjini, Serengeti na Bunda wamesema Nyambari Nyamgwine ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mwaka 2010 hadi 2015, ameshuhudia kuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya jamii katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara.
Hivyo, wengi wao wanatamani kuona akijitokeza kwa mara nyingine kuomba ubunge katika majimbo yao, wakiamini kuwa ni mtu mwenye maono makubwa - yaliyobeba dhamira ya dhati ya kuboresha maisha ya wananchi.
Wametaja mambo yanayofanya wananchi wengi kuvutiwa na Nyambari kuwa ni pamoja na lile la kujitolea kupeleka msaada wa vitabu vya ziada kwenye shule za sekondari zote katika wilaya ya Tarime yenye majimbo mawili ya uchaguzi, yaani Tarime Mjini na Tarime Vijijini.
Wamesema juhudi zake mbalimbali zinazofanywa na Nyambari, zikiwemo hizo za kusaidia kuboresha elimu, zimekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa majimbo hayo.
Hivyo, wananchi wengi wametoa wito kumuomba Nyambari asisite kujitokeza kuwania nafasi ya kuwawakilisha bungeni, kwa kuwa wana imani kubwa na uwezo wake wa kuleta maendeleo ya kisekta katika maeneo yao.
"Nyambari alileta maendeleo makubwa wakati akiwa Mbunge wa Tarime. Mfano, ninakumbuka aliweza kugawa mabati 6,000 katika jimbo zima kwa ajili ya kuezeka majengo ya shule na vituo vya afya,” anasema mkazi wa jimbo la Tarime Vijijini alityejitambulisha kwa jina moja la Nyanswi.
Aidha, Nyambari ameendesha harambee mbalimbali za kuchangia ujenzi wa makanisa wilayani Tarime. Harambee hizo zimedhihirisha upendo wa dhati na moyo wa kujitolea alionao katika kuchangia maendeleo ya jamii, zikiwemo shughuli za kiroho na kiimani.
Pia, wamemtaja Nyambari kuwa ndiye aliyeanzisha wazo la ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) katika kata ya Nyamwaga, hatua ambayo imewezesha huduma za kiutawala kuwa karibu zaidi na wananchi ili kuharakisha maendeleo katika maeneo ya vijijini.
“Hakika Nyambari amejidhihirisha kuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo ya jamii, tutamani ikimpendeza aje kugombea ubunge katika jimbo letu la Tarime Mjini ili atuletee maendeleo ya kijamii na kiuchumi," alisema Amos Manga, mkazi wa Tarime Mjini.

Askofu Amos Muhagachi wa Kanisa la Mennonite Dayosisi ya Shirati akimshukuru Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) kwa kufanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 27 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Mennonite Mangucha katani Nyanungu, Tarime Vijijini hivi karibuni.
-------------------------------------
Wananchi wengine wameshuhudia kuwa Nyambari ni kiongozi wa aina yake, mwenye maono ya kipekee ya maendeleo na ambaye amejaaliwa moyo wa kujitolea kwa hali na mali ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kwa hiyo, wananchi wengi wanamtarajia Nyambari akubali kujitokeza tena katika kinyang'anyiro cha ubunge, ili aendelea aweze kupeleka maendeleo ya kisekta maeneo yao.
"Nyambari ni mfano wa kiongozi mpenda maendeleo, na hilo linathibitishwa na hatua yake ya hivi karibuni ya kujitolea kwa hali na mali katika harambee za kuchangia ujenzi wa makanisa yetu," anasema mkazi wa Tarime Vijijini, Salim Matiko.
"Kwa hakika, Nyambari Nyangwine ni mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa wananchi, anajua shida zetu na anajitahidi kusaidia kuzipatia ufumbuzi kwa vitendo," Matiko aliongeza.
Mkazi wa jimbo la Serengeti, Happy Marwa, anasema “Mchango wa Nyambari katika shughuli za kijamii umeendelea kujenga imani kubwa kwa wananchi wengi wa jimbo hilo na mkoa wa Mara kwa ujumla.”
"Nyambari alipokuwa mbunge aliweza alijizatiti kuhakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa na kuwarahisishia wananchi usafiri," anasema Sophia Chacha, mkazi wa Tarime Vijijini na kuongeza "Sidhani kama mtu mwingine anaweza kufanya zaidi ya alivyofanya."
Naye mkazi wa jimbo la Bunda Mjini, Juma Hassan, anasema “Wananchi wa Bunda tumekuwa tukimuona Nyambari Nyangwine kupitia vyombo vya habari jinsi anavyojitolea kuchangia maendeleo ya jamii katika maeneo mbalimbali. Akija kugombea ubunge huku kwetu hatutamwangusha."
Mwingine aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu kutoka Bunda anasema “Tunatamani kuwa na viongozi aina ya Nyambari Nyangwine, maana ni mtu mwenye upako wa Mungu katika kuchangia maendeleo ya jamii, lakini pia ameonekana kuwa na mvuto wa kisiasa.”
Kwa ujumla, mchango wa Nyambari Nyangwine katika maendeleo ni dhahiri na umeonekana kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Misaada ya hali na mali anayotoa imemjengea uhusiano wa karibu na wananchi, na wengi sasa wanamuona kama lulu inayoweza kuwaletea maendeleo endelevu katika maeneo yao.
Ndiyo maana wananchi wengi hawasiti kusisitiza kwamba Nyambari Nyangwine ana sifa zote za uongozi, hasa katika nafasi ya ubunge, na wanaahidi kumpatia ushirikiano mkubwa iwapo atakubali wito wao wa kujitokeza kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»MAKALA:Bodi ya TANAPA yatilia mkazo ujenzi daraja la Mto Kogatende katika Hifadhi ya Serengeti
»Serengeti: Mwenyekiti UVCCM Mara aunga mkono Serikali kufanikisha upatikanaji wa lishe mashuleni
»MAKALA MAALUMU:Mageuzi makubwa ya maendeleo yashuhudiwa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara
»MAKALA YA UCHAMBUZI:Nyambari Nyangwine ameonesha moyo wa kujitolea na upendo mkubwa katika ujenzi wa makanisa Tarime
No comments:
Post a Comment