
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Wa Mara, Mary Daniel Joseph (katikati) na wenzake wakifurahia tukio la kukabidhi msaada wa masufuria kwa Shule ya Sekondari Koreri.
--------------------------------
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa Wa Mara, Mary Daniel Joseph, ameendelea na ziara yake ya siku tisa, ambapo leo akiwa wilayani Serengeti, amezindua shina la wakereketwa wa chama hicho la Koreri.
Uzinduzi wa shina hilo ni hatua muhimu katika kushawishi vijana kushiriki shughuli za shughuli za maendeleo na ujenzi wa taifa.
Mbali na kuzindua shina hilo, Mary ambaye ameambatana na Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Mara, ameipatia Shule ya Sekondari Koreri msaada wa masufuria yenye thamani ya shilingi milioni 2.5.
Mary ametoa msaada huo wa masufuria ili kuunga mkono ufanikishaji wa upatikanaji wa chakula na lishe shuleni, hivyo kuwezesha wanafunzi kupata elimu bora bila kikwazo cha njaa.
Aidha, Mwenyekiti Mary amekutana na wajasiriamali karika genge la Koreri na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika kuendesha shughuli zao.
Kaulimbiu ya ziara inasema “KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE,” ikilenga kuhamasisha vijana kuchapa kazi na kujali utu wa kila mtu kwa maendeleo ya taifa.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Kazi na Utu: Urithi wa JPM na mustakabali wa taifa letu
»MAKALA:Bodi ya TANAPA yatilia mkazo ujenzi daraja la Mto Kogatende katika Hifadhi ya Serengeti
»MAKALA MAALUMU:Mageuzi makubwa ya maendeleo yashuhudiwa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara
»MAKALA MAALUMU:Nyambari Nyangwine awa lulu mkoani Mara, aombwa kujitokeza kuomba ubunge wakati ukifika
No comments:
Post a Comment