NEWS

Friday, 21 March 2025

Mgodi wa dhahabu wa akinamama wageuka mkombozi kwa vijana wilayani Kahama



Na Nwandishi Wetu


Mgodi wa Dhahabu wa Manda unaomilikiwa na wanawake wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, sasa umeibuka kuwa mkombozi kwa kutoa ajira kwa vijana.


Mgodi huo ulioko kijiji cha Mwime kata ya Zongamela unajivunia kuajiri vijana 200 na kuchangia shilingi milioni 800 katika maduhuli ya serikali kwa mwaka huu wa fedha wa 2024/2025, kwa mujibu wa mmilliki na mwenyekiti wake, Asha Msangi.


Msangi, ambaye kabla ya kujiunga na uchimbaji madini alikuwa akishughulika na biashara ndogo, amewaunganisha wanawake wachimbaji katika kuinua hali zao zs maisha kuuchumi kwa kuunda vikundi vya uchimbaji.


"Nilikuwa nachimba kwenye migodi ya watu na kupata uzoefu. Niliomba leseni na nikapewa moja kama majaribio. Nashukuru nilifanya vizuri na nikaaminika. Sasa hivi namiliki leseni 12," anaeleza mama huyo ambaye sasa amejikita kwenye sekta ya madini.


Afisa Madini Mkazi wa Kahama, Leons Welengeile, anasema Mgodi wa Dhahabu wa Manda ni mdau muhimu kwa serikali kwa sababu umezalisha ajira kwa vijana na wanawake kupitia shughuli mbalimbali zinazofanyika mgodini hapo.


"Kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 kuanzia Julai 2024 hadi Februari 2025 mgodi huu umechangia shilingi milioni 810 katika maduhuli ya serikali kupitia mrabaha na tozo ya ukaguzi, fedha ambazo zinakusanywa na Tume ya Madini hapa Kahama," anasema.


Welengeile anaeleza kuwa fedha nyingine hukusanywa na Halmashauri na Mamlaka ya Mapato.


Kwa mujibu wa Afisa huyo, maduhuli ya serikali katika Mkoa wa Kimadini Kahama yameendelea kupanda mwaka hadi mwaka kutoka shilingi bilioni 97 mwaka 2022/2023 hadi shilingi bilioni 101 mwaka 2023/2024. Kwa mwaka 2024/2025 hadi kufikia mwezi huu wa Machi 2025 kiasi cha shilingi bilioni 88.08 kimekusanywa, sawa na asilimia 85 ya makusanyo ya miezi 9.



"Naamini kwa mwekekeo unavyokwenda mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka tutaweza kutimiza lengo la makusanyo kama ilivyokusudiwa," Welengeile anaeleza.

Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages