
Nyambari Nyangwine akikabidhi tuzo katika hafla ya Tuzo ya Ushairi Chaguo la Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam, Tanzania jana Machi 21, 2025.
----------------------------------------
Huenda washairi wa Tanzania wakapata fursa ya kuonesha vipaji vyao kimataifa kwa kiwango cha juu, baada ya kupata semina maalum ya kuwajengea uwezo zaidi, itakayofadhiliwa na mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, Nyambari Nyangwine.
Nyambari ambaye ni miongoni mwa watu maarufu katika sekta ya fasihi na biashara nchini, alitoa ahadi hiyo wakati akihutubia hafla ya Tuzo ya Ushairi Chaguo la Afrika Mashariki, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Machi 21, 2025.
Katika hotuba yake, Nyambari alisisitiza umuhimu wa kuendeleza na kukuza ushairi wa Tanzania ili kuweza kushindana vyema katika mashindano ya kimataifa.
“Nitawadhamini mfanye semina, nitawaletea manguli waliobobea katika ushairi na fasihi ili muweze kutoa mashairi ambayo hata tunapokwenda kushindana na nchi nyingine tuwe tunawasilisha kitu ambacho kina sifa zote za ushairi,” alisema Nyambari.
Nyambari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliongeza kuwa hatua hiyo itawawezesha kutoa mashairi bora ambayo yataweza kupigiwa mfano hata katika mashindano ya kimataifa.
Kwa kufadhili semina hiyo, Nyambari atachochea mapinduzi katika ushairi wa Kiswahili na kuhamasisha wasomi wengi zaidi kutoka nchi za Afrika Mashariki kuchangia katika kuendeleza ushairi na fasihi katika mazingira ya kisasa.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Tarime Vijijini: Wananchi Nyanungu walia ubovu wa barabara ya kwenda zahanati ya Nyandage
»Taasisi ya Mwanzo Mpya yawanoa wanawake Tarime, yampongeza Rais Samia
»Namibia yamuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke, Rais Samia ampongeza
»Serengeti: Mwenyekiti UVCCM Mara aunga mkono Serikali kufanikisha upatikanaji wa lishe mashuleni
No comments:
Post a Comment