NEWS

Wednesday, 12 March 2025

Motsepe achaguliwa tena kuwa rais wa CAF kwa muhula mwingine


Patrice Motsepe amechaguliwa tena bila kupingwa kuwa rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ikiwa ni muhula wake wa pili madarakani.

Raia huyo wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 63, ambaye amekuwa rais wa Caf tangu 2021, alitangaza uamuzi wake wa kugombea tena Oktoba 2024.

Kuchaguliwa kwake tena kwa muhula mwingine wa miaka minne kulithibitishwa katika mkutano mkuu wa wa Caf mjini Cairo uliofanyika leo Jumatano uliohudhuriwa pia na rais wa Fifa Gianni Infantino.

Motsepe, gwiji wa madini ambaye pia anamiliki klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, alisema anatazamia kuendeleza "maendeleo mazuri" aliyoyafanya tangu aingie madarakani miaka minne iliyopita.

Kwa upande wa jumbe wa lama kamati kuu ya Caf, nguli wa soka wa Cameroon Samuel Eto'o ameshinda nafasi ya ujumbe.

Wawakilishi wa bara hilo kwenye baraza la Fifa pia walipigiwa kura wakati wa mkutano mkuu huo wa utendaji wa Jumatano.

Kukosekana kwa washindani kwenye nafasi ya Motsepe, ni kama Nchi nyingi kupitia mashirikisho yao yanamuunga mkono hasa baada ya kuingia Caf wakati ikiwa na matatizo mengi, ambayo hayaonekani kwa sasa, ikiwemo fedha na utawala.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages