NEWS

Wednesday, 12 March 2025

Tarime: Sinda amuunga mkono Nyambari uchangiaji fedha za ununuzi vifaa vya kwaya ya EAGT Sirari Bondeni



Sinda Samson Mseti

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Mdau wa maendeleo, Sinda Samson Mseti, amemuunga mkono Nyambari Nyangwine kwa shilingi 400,000 katika uchangiaji fedha za kununua vyombo vya muziki vya kwaya ya Kanisa la EAGT Sirari Bondeni.

Sinda alimsindikiza kwa kiasi hicho cha fedha kanisani hapo wiki iliyopita, wakati Nyambari alipoichangia kwaya hiyo shilingi milioni mbili taslimu kwa ajili ya kufanikisha ununuzi wa vifaa hivyo.

Katika usindikizaji huo, Sinda aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kanisani, Nyangi Barnabas.

Nyambari Nyangwine (katikati) akikabidhi msaada wa shilingi milioni mbili kanisani hapo.
-------------------------------------



Taarifa zilizotufikia kutoka kanisani hapo zinasema tayari kwaya hiyo imeshanunua kinanda kipya kutokana na mchango huo wa Nyambari na Sinda.

Nyambari Nyangwine ni mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara kupitia chama tawala - CCM mwaka 2010 hadi 2015.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages