NEWS

Wednesday, 5 March 2025

RCC Mara yabariki pendekezo la kugawa jimbo la Serengeti




Na Mwandishi Wetu, Musoma

Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa Mara imepitisha kwa kauli moja pendekezo la kuligawa jimbo la uchaguzi la Serengeti ili kupata majimbo mawili.

Majimbo hayo ni Serengeti Mashariki litakaloundwa na kata 14 na Serengeti Magharibi lotakalokuwa na kata 16.

Wakichangia hoja katika kikao cha RCC kilichofanyika mjini Musoma leo Jumatano, wachangiaji wote wamekubalina na umuhimu wakugawa jimbo hilo lenye kata 30.

Hoja hiyo imejadiliwa baada ya kupitishwa kwenye vikao vya kisheria wilayani Serengeti, na baada ya kupitishwa na RCC sasa suala hilo litawasilishwa kwenye Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya maamuzi.

Kikao hicho cha RCC kilihudhuriwa naviongozi wakuuwa mkoa huo akiwemo  Mwenyekitiwa chama-tawala CCM, Patrick Chandi Marwa na kuongozwa na Mkuu wa Mara, Kanali Evans Mtambi. 

Jana Jumanne, Baraza la Madiwani na Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) ya Serengeti kwa kauli moja walipitisha rasmi pendekezo la kugawa jimbo la Serengeti kuwa majimbo mawili, baada ya kukusanya maoni ya wananchi kutoka kata zote 30, taasisi mbalimbali na vyama vya siasa.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages