
Prof Philemon Sarungi enzi za uhai
Na Mwandishi Wetu
Waziri mstaafu na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Rorya mkoani Mara, Prof Philemon Sarungi, amefariki dunia jijini Dar es Salaam, Tanzania akiwa na umri wa miaka 89.
Msemaji wa familia ya Chifu Sarungi, Martin Sarungi aliviambia vyombo vya habari kwamba Prof Sarungi aliaga dunia akiwa nyumbani kwake Oysterbay, Msasani jana Machi 5, 2025 saa 10 jioni.
Kwa mujibu wa Martin, Prof Sarungi amefikwa na mauti siku chache baada ya kuugua malaria na kupata nafuu.
Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam wakati ratiba za shughuli za mazishi zikisubiri watoto na wajukuu ambao wengi wako nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment