
Kepteni Sharifu Nyengedi wa JWTZ Kikosi cha Nyandoto - Tarime, akizungumza katika semina maalum kwa wanawake iliyoendeshwa na Taasisi ya Mwanzo Mpya mjini Tarime jana Machi 22, 2025.
--------------------------------
Taasisi ya Mwanzo Mpya (MMF) imeendesha semina maalum kwa wanawake zaidi ya 500 kutoka makundi mbalimbali wilayani Tarime, Mara.
Semina hiyo iliyokuwa na kaulimbiu isemayo "Mwanzo Imara, Mwanamke Imara", ilifanyika mjini Tarime jana Machi 22, 2025, ambapo wanawake hao walipatiwa elimu ya malezi na makuzi kwa watoto, madhara ya dawa za kulevya na namna ya kukua kiuchumi.
Ilielezwa kuwa semina hiyo ni sehemu ya kutambua na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele ambaye aliwakilishwa na Kepteni Sharifu Nyengedi wa JWTZ Kikosi cha Nyandoto - Tarime, aliwambia alisema mwanamke ana haki ya kuwa na shughuli ya kujipatia kipato kama ilivyo Kwa mwanaume.
Aidha, aliwahimiza wanawake kuchangamkia mikopo inayaotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kufanya biashara na kujiletea maendeleo.
"Chukueni mikopo hiyo mkafanye biashara na mpate faida. Ukimuinua mwanamke kiuchumi anakuwa na nguvu kiuchumi, kijamii na kisiasa. Taasisi hii [MMF] imekuja kwa muda mwafaka - inazungumza kuhusu maendeleo ya akina mama," alisema.

Kepteni Nyengedi akikabidhi vyeti.
----------------------------
Awali, Mkurugenzi wa MMF, Mussa Ryoba limpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa aliyofanya kwa kuwaletea wananchi maendeleo ya kisekta kwa kipindi kifupi cha miaka minne.
"Sisi kipaumbele chetu ni mama [Rais Samia], tutamshika - tutashirikiana naye kwa hali na mali kuhakikisha kwamba kura atakazopata nyingi - moja ya wilaya itakayosemwa ni Tarime na Kanda ya Ziwa kwa ujumla,” alisema Ryoba na kuwahimiza washiriki wa semina hiyo kuwa mabalozi wazuri Kwa kutangaza maendeleo yaliyoletwa na Rais Samia.
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Mvua yaharibu nyumba, miundombinu Musoma Mjini, baadhi ya watu wakosa makazi
»Tarime Vijijini: Wananchi Nyanungu walia ubovu wa barabara ya kwenda zahanati ya Nyandage
»Nyambari Nyangwine kufadhili semina ya washairi wa Tanzania ili kuboresha ufanisi wao
»Namibia yamuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke, Rais Samia ampongeza
No comments:
Post a Comment