
Na Mwandishi Wetu, Musoma
Kaya zaidi ya 60 katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara hazina mahali pa kuishi baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuezua paa za nyumba zao usiku wa kuamkia leo Machi 24, 2025.
Pia, mvua hiyo imeezua paa za majengo ya taasisi mbalimbali, zikiwemo shule za msingi, kituo cha polisi, msikiti na kuharibu baadhi ya miundombinu ya umeme, barabara na majengo ya biashara.
Aidha, watu wanne wameripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo.
Diwani wa Kata ya Kitaji, Golden Marcus, alisema tathmini inafanyika ili kujua hasara iliyosababishwa na maafa hayo.
Naye Mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Mathayo, ametembelea eneo la tukio kujionea uharibifu uliotokea.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka amewataka wananchi katika eneo hilo kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na utaratibu wa kuhakikisha kila kitu kinarejea katika hali ya kawaida.
Hadi taarifa hii inachapishwa, serikali ilikuwa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hasara iliyosababishwa na maafa hayo.
Mji wa Musoma, ambao kwa miaka ya hivi karibuni umeshuhudia kasi kubwa ya ukuaji wake uko kandokando ya Ziwa Victoria ambalo limeleta fursa za kiuchumi kwa sekta ya uvuvi.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Tarime Vijijini: Wananchi Nyanungu walia ubovu wa barabara ya kwenda zahanati ya Nyandage
»Nyambari Nyangwine kufadhili semina ya washairi wa Tanzania ili kuboresha ufanisi wao
»Namibia yamuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke, Rais Samia ampongeza
»Serengeti: Mwenyekiti UVCCM Mara aunga mkono Serikali kufanikisha upatikanaji wa lishe mashuleni
No comments:
Post a Comment