NEWS

Wednesday, 2 April 2025

Askari Magereza wawili mbaroni mwa Polisi kwa mauaji ya mwanakijiji wilayani Serengeti




Na Mwandishi Wetu

Askari wa Jeshi la Magereza Tabora B, Sijali William Hence na Ilinus Mushumbushi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mkazi wa kijiji cha Kisangura wilayani Serengeti, Emmanuel Lucas Chacha (18).

Wanadaiwa kusababisha kifo hicho Machi 31, 2025 saa nne asuhuhi ndani ya mradi wa ufugaji katika Gereza la Tabora B, baada ya kukamata ng’ombe 98, mbuzi watano na kondoo sita walioingizwa eneo hilo kinyume cha sheria.

Wakati wa jitihada za kupeleka mifugo hiyo kuhifadhiwa ndani ya kambi ya mradi huo, ghafla vijana zaidi ya 20 kutoka uraiani waliwavamia askari waliokuwa zamu na kuwashambulia kwa silaha za kijadi.

Ndipo katika juhudi za kujiokoa, askari hao walifyatua risasi kadhaa hewani kwa lengo la kutawanya kundi hilo la vijana, Emmanuel Lucas Chacha alijeruhiwa na kufariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitalini.

“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya mauaji hayo,” ilisema taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, huku likiwataka wananchi kuheshimu mipaka ya malisho ya mifugo kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages