NEWS

Wednesday, 2 April 2025

Makamu wa Rais awataka wakimbiza Mwenge wa Uhuru kufichua ubadhirifu wa fedha za umma



Makamu wa Rais, Dkt Philip Isdor Mpango, akikabidhi Mwenye wa Uhuru kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge huo Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, mkoani Pwani leo Machi 2, 2025.
--------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Isdor Mpango, amewataka viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 kumulika na kifichua bila woga vitendo vyote vibaya, vikiwemo vya ubadhirifu wa fedha za umma katika kila halmashauri watakayopita nchini.

Dkt Mpango ametoa maelekezo hayo kupitia hotuba yake ya uzunduzi wa mbio hizo mkoani Pwani leo Aprili 2, 2025.

Aidha, Dkt Mpango ameziagiza mamlaka za serikali za mitaa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru ili weweze kutimiza lengo lililokusudiwa.

Makamu wa Rais, Dkt Philip Isdor Mpango, akiwasha Mwenye wa Uhuru wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge huo mkoani Pwani leo Machi 2, 2025.
-------------------------------

Mwenge huo wa uhuru utakimbizwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195 kuanzia leo na kuhitimishwa mkoani Mbeya Oktoba 14, 2025.

Kiongozi wa mbio za Mwege wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 ni Ismail Ali Ussi kutoka Kaskazini Unguja.

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 inasema “Jitokeze Kushuriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu”.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages