
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, akikabidhi mpira wakati kuzindua mashindano ya UMITASHUMITA Mkoa wa Mara juzi Aprili 9, 2025.
-----------------------------------
Na Godfrey Marwa, Tarime
Mashindo ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMITA) ngazi ya mkoa, yamezinduliwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Tarime iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Mashindano hayo yalizinduliwa juzi Aprili 9, 2025, ambapo wanamichezo zaidi ya 1,000 kutoka halmashauri tisa za mkoa wa Mara wanashirki michezo mbalimbali ili kupata timu moja kwa kila mchezo itakayowakilisha mkoa kwenye mashindano ya kitaifa baadaye mwaka huu.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, aLIwataka waandaaji wajitahidi kupata timu bora itakayowakilisha mkoa vizuri na hatimaye kushinda na kuuletea mkoa heshima.
Aidha, Meja Gowele aliwataka wanamichezo hao kudumisha nidhamu katika kipindi chote cha mashidano hayo kwa kuwa michezo ni afya, ajira na fursa kwa kila mmoja kuonesha kipaji chake.
Naye Kaimu Mkuu wa kitengo cha utamaduni sanaa na michezo wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Mwalimu Teddy Msyangi, aliwakaribisha wanafunzi, wananchi na wadau wa nichezo kujitokeza kushiriki na kushuhudia burudani za mashindano hayo.
"Tunawaomba wadau mbalimbali wakiwemo vingozi na wafanyabiashara kujitokeza kusapoti michezo hii kama vike kujenga miundombinu ya michezo kwa faida ya watoto wetu, michezo ni fursa inayolipa sana hapa ulimwenguni," alisema Mwalimu Teddy.
No comments:
Post a Comment