
Wachezaji wa Simba SC, Mpanzu (kushoto) na Kibu wakishangilia ushindi dhidi ya Al Masry jijini Dar es Salaam leo Aprili 9, 2025.
-----------------------------------
Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Soka ya Simba kutoka Tanzania imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya Nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025, baada ya kuifungasha virago Klabu ya Al Masry kutoka Misri, kwa mikwaju ya penati 4-1.

Simba imeibuka na ushindi huo mnono katika mechi ya marudiano iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania leo Aprili 9, 2025.

Kutokana na ushindi huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Simba na kuitakia kila la heri katika hatua inayofuata ya nusu fainali ya mashindano hayo.
“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali,” Rais Samia ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii.

No comments:
Post a Comment