NEWS

Tuesday, 6 May 2025

Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/25: Simba, Yanga sasa kumenyana Juni 15




Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imetoa ratiba mpya ya mwendelezo wa michezo ya ligi hiyo ambapo mechi ya Simba na Yanga "Kariakoo Derby" imepangwa kufanyika Juni 15, 2025 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.

Ratiba hiyo imefanyiwa marekebisho ili kutoa nafasi kwa ajili ya mechi hiyo ya Watani wa Jadi ambayo iliahirishwa Machi 8, 2025 kutokana na sintofahamu iliyojitokeza siku moja kabla ya mchezo huo.

Hata hivyo, mashabiki wa soka nchini wameonesha kuwa na wasiwasi juu ya uwepo wa mechi hiyo kutokana na msimamo wa kutoshiriki uliotolewa jana na Klabu ya Yanga.

Ikumbukwe kuwa Yanga ilipeleka shauri mbele ya mahakama ya kimataifa ya michezo "CAS" ikipinga uamuzi wa kuahirishwa kwa mchezo huo, lakini CAS ikaijibu Yanga kuwa inapaswa kuanzia kwenye mamlaka za ndani - jambo ambalo lilipingwa vikali na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages