![]() | |
-------------------------- |
NA MWANDISHI WETU
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Rais wa Masuala ya Afya, Prof. Mohamed Yakub Janabi, amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika katika uchaguzi uliofanyika jana jijini Geneva, Uswisi.
Profesa Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mtanzania mwingine aliyekuwa Mkurugenzi Mteule, Dkt. Faustine Ndugulile, ambaye alifariki dunia Novemba 2024 kabla ya kuitumikia nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya WHO iliyotolewa jana baada ya kufanyika uchaguzi wa mrithi wa nafasi hiyo, Prof. Janabi alichuana na wagombea wengine wanne na kutofanikiwa. Wagombe hao ni Prof. Moustafa Mijiyawa wa Togo, Dkt. N’Da Konan Michel Yao wa Ivory Coast, Dkt. Boureima Hama Sambo wa Niger na Mohamed Lamine Drame wa Guinea.
Kwa mujibu wa utaratibu wa WHO, Prof.. Janabi atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha mwisho cha miaka mitano.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana alimpongeza Prof. Janabi kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo mpya ya kulitumikia bara la Afrika katika sekta ya afya.
Katika salaam za pongezi alizomtumia bingwa huyo wa afya, Rais Samia alisema miongo ya ubobezi na uzoefu katika sekta ya afya ndiyo iliyombeba .
“Ni imani yangu kwamba una kila kitu cha kulitumikia bara letu na kutuongeza sote kwenye kilele cha ubora wa huduma za afya,” Rais Samia alisema katika salaam hizo.
“Tanzania inaishukuru kila nchi ambayo iliamini katika ujuzi na uzoefu wako na dira ya bara letu," aliongeza.
Prof. Janabi ni bingwa wa masuala ya afya ambaye ameleta mageuzi makubwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hasa kuhusu ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa na kuwa muasisi wa tiba ya magonjwa ya moyo ambayo zamani ilibidi wagonjwa wapelekwe nchi za nje kama India kwa ajili ya matibabu
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika inayojivunia kuwa wataalam wengi wa afya ambao wanafanya kazi nje ya nchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali imefanya jitihada kubwa za kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ili kuwarejesha wataalamu wake wengi katika fani mbalimbali ambao walikuwa nje ya nchi.

No comments:
Post a Comment