
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo ameongoza orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaolipwa fedha nyingi zaidi kwa mwaka wa tatu mfululizo, huku nyota wa NBA, Stephen Curry akipanda hadi nafasi ya pili.

Stephen Curry
Jarida la biashara la Forbes linasema Ronaldo ambaye ameongoza orodha hiyo mara tano wakati wa uchezaji wake, ameongeza mapato yake yote kwa $15m hadi $275m (takriban £206m).
Idadi hiyo imezidiwa tu na bondia bingwa wa zamani wa dunia, Floyd Mayweather, ambaye alipata $300m mwaka 2015 (wakati huo £194m) na $275m mwaka 2018 (£205m).
Mshambulizi wa Ureno, Ronaldo, mwenye umri wa miaka 40, alihamia kwenye Ligi ya kifahari ya Saudi Pro League akiwa na Al Nassr Desemba 2022 na amejipatia mapato makubwa kupitia uidhinishaji nje ya uwanja na mikataba ya udhamini inayoungwa mkono na wafuasi wake wa mitandao ya kijamii - ambao kwa sasa wanafikia milioni 939.
Mlinzi wa Golden State, Warriors Curry, ambaye alikua mchezaji wa kwanza wa NBA kufikisha pointi 4,000 katika taaluma yake Machi, alipanda hadi wa pili baada ya kupata $156m (takriban £117m).
Bondia wa Uingereza, Tyson Fury, alipanda hadi wa tatu kwa $146m (takriban £109m) licha ya kupoteza mataji yake ya uzito wa juu kwa Oleksandr Usyk wa Ukraine mwezi Desemba.
Fury alifaidika na kipindi cha uhalisia cha televisheni cha Netflix na ushirikiano na utalii wa Malta. Mpinzani wa muda mrefu wa Ronaldo, Lionel Messi, amezidi kuwa nyuma ya Mreno huyo baada ya kushuka kutoka nafasi ya tatu hadi ya tano.
Wanamichezo 10 bora wanaolipwa fedha nyingi zaidi 2025 ni wafuatao:
1. Cristiano Ronaldo - Soka: $275m (£206.6m)
2. Stephen Curry - Mpira wa vikapu: $156m (£117.2m)
3. Tyson Fury - Ndondi: $146m (£109.7m)
4. Dak Prescott, American football: $137m (£103m)
5. Lionel Messi- Soka: $135m (£101.4m)
6. LeBron James - Mpira wa vikapu: $133.8m (£105.5m)
7. Juan Soto - baseball: $114m (£85.7m)
8. Karim Benzema- Soka: $104m (£78.2m)
9. Shohei Ohtani- baseball: $102.5m (£77m)
10. Kevin Durant - Mpira wa vikapu: $101.4m (£76.2m)
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment