
Elizabeth Thomas Msabi (kulia) kutoka UK akiwa katika picha ya pamoja na wana-Diaspora wenzake wakihudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa jijini Dodoma leo Mei 29, 2025.
-------------------------------------------
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, wana-Diaspora (Watanzania wanaoishi ughaibuni) wamealikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushiriki Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Miongoni mwa Diaspora hao kutoka mataifa mbalimbali, wamo 10 kutoka Uingereza (UK) akiwemo Elizabeth Thomas Msabi, kuhudhuria mkutano huo unaofanyika jijini Dodoma leo Mei 29, 2025.
Tukio hilo limetazamwa kama hatua ya kihistoria na ya kipekee katika kujumuisha Watanzania waishio nje ya nchi katika masuala ya kitaifa.

Elizabeth Thomas Msabi akishiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa jijini Dodoma.
----------------------------------------

Wana-Diaspora wanachama wa CCM kutoka London, Uingereza, Elizabeth Thomas Msabi (kulia) na mwenzake wakionesha bango lao.
---------------------------------------
Elizabeth amemshukuru Rais Samia kwa hatua ya kipekee ya kuwakumbuka na kuwathamini Watanzania wanaoishi ughaibuni na kuwapatia heshima kubwa ya kuwaalika kushiriki mkutano huo.
Amesema hadhi waliyopewa si tu heshima kwao binafsi, bali ni ishara ya kuthamini mchango wao katika taifa, na inawapa moyo wa kufikiria kurudi Tanzania ili kusaidia juhudi za ujenzi wa taifa lao katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
"Tunamshukuru sana Rais wetu Dkt Samia kwa kuwakumbuka Watanzania waishio nje ya nchi, hali ambayo imewapa hamasa na moyo wa kurudi nyumbani kumsaidia Rais na Watanzania wenzao katika kutumikia na kuendeleza ujenzi wa taifa lao walipendalo sana,” amesema Elizabeth katika mazungumzo na Mara Online News.
Ushiriki wa wana-Diaspora kutoka mataifa mbalimbali katika Mkutano Mkuu huo wa CCM Taifa ni kielelezo kuwa Tanzania inaendelea kuimarika chini ya uongozi thabiti wa Rais Samia, na kuchochea mshikamano wa kitaifa na maendeleo jumuishi.
No comments:
Post a Comment