NEWS

Friday, 25 July 2025

CCM yaitisha Mkutano Mkuu Maalum kufanya marekebisho madogo ya Katiba yake



Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) jijini Dodoma leo.
----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitisha Mkutano Mkuu Maalum utakofanyika kesho Julai 26, 2025 kwa njia ya mtandao, huku ajenda kuu ikitajwa kuwa ni marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho tawala.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amesema katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo kwamba maabdalizi ya mkutano huo yamekamilika.

Makalla amesema kumekuwepo na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano huo, akisisitiza kuwa Katiba ya chama hicho inawaruhusu kufanya mkutano mkuu maalum kwa njia ya mtandao pale wanapoona inafaa.

"Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100, wilaya zipo tayari, mikoa yote ipo tayari, Sekretarieti tunaendelea na maandalizi ili kufanikisha mkutano huu mkuu maalum ambao utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM," amesema.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages