NEWS

Sunday, 6 July 2025

Kishindo cha Makuri nia ya ubunge Serengeti kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025



Paul Chacha Makuri

Na Mchambuzi Wetu, Serengeti

Macho na masikio ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla kwa sasa yameelekezwa zaidi kwa watia nia za ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Miongoni mwa watia nia za ubunge waliojitokeza kipindi hiki cha michakato ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ni kada kijana wa CCM, Paul Chacha Makuri, anayewania kiti cha ubunge katika jimbo la Serengeti, mkoani Mara.

Makuri anatajwa kuwa na nguvu ya ushawishi ndani na nje ya chama hicho tawala katika jimbo la Serengeti, akiwakilisha kizazi kipya kwa matumaini na ari mpya.

Ni kijana mzaliwa wa Serengeti, ambaye mwaka huu ametangaza kwa kishindo nia ya ubunge wa jimbo hilo kwa mara ya pili baada ya kujitokeza mwaka 2020 bila mafanikio, akisaka ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kuelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amekuwa akikaririwa kutaja vipaumbele vyake vikuu vinavyomsukuma kuwania ubunge wa Serengeti kuwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, kuhakikisha afya na elimu bora vijijini, kuwezesha vijana kwa ajira na mitaji na kupambana na umasikini wa kipato.

Safari yake ya kisiasa inatajwa kujengwa katika misingi ya uzalendo, mshikamano wa kijamii na kujitolea kwa maslahi mapana ya umma.

Amejitokeza kwa kishindo, ‘akipigiwa saluti’ na kundi kubwa la wananchi - vijana, wanawake na wazee ndani na nje ya CCM, ambao wanaona ndani yake dira ya matumaini mapya kwa mustakabali mwema wa jimbo la Serengeti.

Anatazamwa kama alama ya kizazi cha sasa, anayewakilisha vijana wanaohitaji nafasi kwa ajili ya kuleta maendeleo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi wote.

Kwa ujumla, Makuri anaonekana kuwa chaguo la kizazi kipya kinachotaka mabadiliko yenye msingi wa kazi na uwajibikaji kwa maendeleo ya kisekta katika jimbo la Serengeti.

Mbali na Paul Chacha Makuri, wanachama wa CCM waliojitokeza kutia ni ya ubunge katika jimbo la Serengeti, ni pamoja na Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Wakili Michael Mahende, Mary Joseph Daniel, Dkt. Amsabi Mrimi na Deograrius Chacha, miongoni mwa wengine.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages