NEWS

Saturday, 9 August 2025

Dodoma: Dkt. Samia achukua fomu ya INEC ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM



Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele (wa pili kulia), akimkabidhi Dkt. Samia Suluhu Hassan, jijini Dodoma leo mkoba wenye fomu ya uteuzi wa kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM. Wengine ni mgombea mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhani.
---------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amechukua kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) fomu ya uteuzi wa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Samia ambaye amefuatana na mgombea mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele, kwenye ofisi za tume hiyo jijini Dodoma leo.

Dkt. Samia na Balozi Dkt. Nchimbi wakionesha mkoba wenye fomu ya uteuzi wa kugombea Urais na Makamu wa Rais.

Kulingana na ratiba iliyotangazwa na INEC, uchukuaji wa fomu za uteuzi wa kugombea kiti cha Urais na Makamu wa Rais ni kuanzia leo Agosti 9 hadi 27, 2025.

Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini zitafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28, kabla ya uchaguzi wenyewe utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages