NEWS

Friday, 8 August 2025

RC Mara aongoza Maadhimisho ya Nanenane 2025 Kanda ya Ziwa Mashariki



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi akitembelea mashamba darasa kwenye Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu leo.
------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Bariadi

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi, leo amewaongoza viongozi na wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima - Nanenane 2025 yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

Baada ya kuwasili Nyakabindi, Kanali Mtambi amepokea taarifa kabla ya kukagua mashamba darasa na mabanda ya maonesho ya bidhaa na zana za kilimo - kutoka mikoa ya Mara, Shinyanga na Simiyu.

Kanali Mtambi ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha na viongozi wengine wa serikali na vyama vya siasa.

Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nanenane Nzuguni, Mji Mkuu wa Serikali, jijini Dodoma, mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo pia kuzindua Maabara Kuu ya kisasa ya Kilimo.

Maonesho ya Nanenane ni hafla ya kila mwaka inayofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8 kila mwaka kutambua na kuthamini mchango wa wakulima katika uchumi wa Taifa, ikishirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali zinazohusiana na kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili.

Kupitia Maadhimisho hayo, wadau huonesha bunifu, teknolojia na kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuongeza tija, uzalishaji na uendelevu wa kilimo.

Mwaka huu wa 2025, Tanzania inaadhimisha Maonesho ya 32 ya Nanenane yenye hadhi ya Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza uchumi, kuongeza matumizi ya teknolojia bora na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages