NEWS

Wednesday, 27 August 2025

Jackson, Mwera, Ruge wapaisha joto la uchaguzi Mara


Na Mwandishi Wetu, Mara

Jackson Kangoye, Charles Mwera na Catherine Ruge, ni miongoni mwa wanasiasa waliochukua fomu za kugombea ubunge mkoani Mara kupitia ACT- Wazalendo na CHAUMMA kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Mwanasiasa kijana Jackson Kangoye amepaisha joto la uchaguzi Tarime Mjini baada ya kuhama chama tawala – CCM na kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia ACT- Wazalendo.

Jackson Kangoye (kushoto) akipokea fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya ACT- Wazalendo.
--------------------------------------

Charles Mwera ambaye amepata kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (kabla halijagawanywa kuwa majimbo mawili) kupitia CHADEMA, naye amevuta hisia za watu kwa kujitokeza kugombea ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya ACT- Wazalendo.
Charles Mwera (kulia) akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia ACT- Wazalendo.
-------------------------------------

Naye Mwanamama jasiri, Catherine Ruge, amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Serengeti kwa tiketi ya CHAUMMA – akiahidi kuwa tayari kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa weledi wa hali ya juu.

Catherine Ruge (kulia) akichukua fomu ya CHAUMMA ya kugombea ubunge jimbo la Serengeti.
--------------------------------------

Kuchukua fomu za ubunge kwa watatu hao kunatajwa na uongozi wa ACT- Wazalendo na CHAUMMA kwamba wanasiasa hao ni chachu ya mabadiliko kwenye majimbo husika.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages