NEWS

Wednesday, 27 August 2025

Wagombea ubunge Mara wachukua fomu tayari kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025



Prof. Sospeter Muhongo akionesha fomu yake ya uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Musoma Vijijini jana.
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Mara

Baadhi ya wagombea ubunge mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana walikamilisha mchakamchaka wa kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo tayari kwa kampeni zitakazoanza rasmi kesho tayari kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Mkoa wa Mara una majimbo 10 ya uchaguzi; ambayo ni Rorya, Bunda Mjini, Serengeti, Musoma Vijijini, Musoma Mjini, Tarime Vijijini, Tarime Vijijini, Bunda Vijijini, Mwibara na Butiama.

Wagombea wa CCM waliochukua fomu jana ni pamoja na Prof. Sospeter Muhongo anayetetea ubunge katika jimbo la Musoma Vijijini, Dkt. Wilson Charles Mahera anayegombea kwa mara ya kwanza kiti cha ubunge jimbo la Butiama lililokuwa likiongozwa na Jumanne Sagini.

Wagombea wengine waliochukua fomu ni Esther Matiko aliyeteuliwa na CCM kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Mjini na Mary Daniel Joseph ambaye kwa mara ya kwanza anagombea ubunge jimbo la Serengeti.

Dkt. Wilson Charles Mahera (kulia) akionesha fomu yake ya uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Butiama jana.
------------------------------------

Mgombea Ubunge Jimbo la 
Tarime Mjini, Esther Matiko.
-------------------------------------

Wagombea ubunge, Mgore Miraji Kigera (kushoto) na Mary Daniel Joseph.
--------------------------------------

Inatarajiwa kwamba wagombea wa majimbo mengine ya mkoa wa Mara kupitia CCM watakamilisha uchukuaji fomu leo Jumatano ili kuanza mikikimikiki ya kampeni za kupambana na wagombea wa vyama vingine.

Kwa mkoa wa Mara, wagombea ubunge wa majimbo wanaojaribu bahati yao kwa mara ya kwanza ya kupata ridhaa ya kuwakilisha wananchi bungeni ni Mary Daniel Joseph wa Serengeti, Dkt. Wilson Mahera wa Butiama na Mgore Miraji Kigera wa Musoma Mjini.

Mgombe mwingine, Kangi Lugola wa jimbo la Mwibara anajaribu tena bahati yake kwa mara nyingine kwa kuwa aliwahi kushika nafasi hiyo na kufanikiwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages